RUCUSORudi nyumbani
RUCUSO · rucuso.online

Sera ya Faragha

Ilisasishwa:

Ukurasa huu unaeleza jinsi taarifa zinavyotumika katika huduma za RUCUSO kwenye rucuso.online.

1. Taarifa zinazochakatwa

Unapochagua kuingia kwa Google, Supabase Auth hupokea utambulisho wa akaunti yako, kama jina, email, kitambulisho cha akaunti na picha ya wasifu inayotolewa na Google. Taarifa hizi hutumika kuingia na kusimamia ruhusa za akaunti. Hatukuombi password ya Google kwenye RUCUSO, wala ruhusa ya kusoma Gmail, mafaili ya Google Drive au contacts zako.

Fomu zinaweza kukusanya jina, kozi, mwaka wa masomo, reg. number inapohitajika, simu, email, maoni na viambatisho unavyochagua kuwasilisha. Ripoti za vitu vilivyopotea au kupatikana zina taarifa za tukio, hostel au eneo unaloishi na mawasiliano yako. Maoni ya mwaka wa kwanza yana taarifa zinazojazwa na mtumaji na hazihesabiwi kuwa zimethibitishwa na database.

Maombi ya chat yana jina linaloonekana, kozi, mwaka na reg. number kwa miaka inayohitajika. Ujumbe wa chat na ripoti za ujumbe huhifadhiwa. Study Hub huhifadhi maelezo na links za materials au maombi unayotuma. Kurasa za viongozi zinaweza kuonyesha taarifa zao zilizochaguliwa kuchapishwa.

Usajili wa michezo wa tukio la sasa

Usajili wa michezo hukusanya majina matatu, reg. number, simu, course, mwaka wa masomo, jinsia na michezo uliyochagua. Waziri na Naibu wa Michezo na super admin pekee wana ruhusa ya kuona orodha na kupakua Excel/PDF kwa kupanga washiriki na kuwasiliana kuhusu tukio. Katibu na wanafunzi wengine hawaonyeshwi taarifa hizo. Idadi ya washiriki pekee inaweza kuonekana kwa umma. Taarifa hizi zinajazwa na mwanafunzi; fomu haihakiki kuwa reg. number ipo kwenye orodha ya chuo.

Maoni ya Elimu na uthibitisho wa cheo

Sehemu ya Elimu hukusanya majina, reg. number, course, mwaka, simu, cheo anachojitambulisha nacho mtumaji, maelezo na link ya ushahidi anayoamua kushiriki. Waziri na Naibu wa Elimu na super admin pekee huona na kujibu taarifa hizi. Super admin anaweza kuunganisha akaunti ya CR au Mbunge na rekodi iliyohakikiwa; Waziri huthibitishwa kutoka akaunti ya uongozi. Cheo cha kujitambulisha hakitoi ruhusa za mfumo. Majibu yanafuatiliwa kwa namba ya kumbukumbu na msimbo wa siri. Links za ushahidi ziko kwenye huduma za mwenye faili, na ruhusa zao zinabaki chini ya mwenye faili.

2. Tunazitumia kwa nini

Taarifa hutumika kushughulikia maoni na ripoti, kuwasiliana na mtumaji, kuonyesha maendeleo ya kesi, kukagua uanachama wa chat, kusimamia ujumbe na kuchapisha materials zilizokubaliwa. Google login peke yake haithibitishi kuwa mtu ni mwanafunzi wa RUCU. Taarifa za utambulisho wa Google hazitumiki kuomba ufikiaji wa Gmail au Drive, na huduma hizi haziombi ruhusa hizo.

Taarifa za kiufundi za maombi ya mtandao, kama IP na muda wa ombi, zinaweza kuchakatwa na hosting na watoa huduma kwa uendeshaji, kumbukumbu za hitilafu na kuzuia matumizi mabaya.

3. Nani anaweza kuona taarifa

Ripoti za ulinzi huonekana kwa Waziri na Naibu wa Ulinzi na super admin pekee. Maoni yanayochagua wizara huonekana kwa Waziri na Naibu wa wizara hiyo na super admin pekee; jambo lisilochagua wizara huenda kwa super admin. Katibu, viongozi wa wizara nyingine na admin wa kawaida hawapewi ufikiaji wa taarifa hizi. Majibu ya maoni mapya yanahitaji kumbukumbu na msimbo wa siri; kumbukumbu za zamani bila msimbo huonesha hali pekee. Namba ya kumbukumbu na msimbo wa siri vinahitajika kufuatilia ripoti mpya za huduma za wanafunzi; hifadhi msimbo huo kwa faragha.

Wanachama walioruhusiwa wa chat huona jina ulilochagua, ujumbe na muda wake. Reg. number, email na simu za akaunti hazichapishwi kama sehemu ya ujumbe wa group. Ukiziandika mwenyewe kwenye ujumbe, wanachama wengine wanaweza kuziona. Materials na maombi ya Study Hub yaliyochapishwa huonekana kwa umma. Taarifa za mawasiliano za viongozi huchapishwa kulingana na mipangilio ya uchapishaji.

Wasimamizi wenye ruhusa wanaweza kukagua maombi, ujumbe na ripoti zinazohusiana na majukumu yao. Usishiriki PIN, password, namba kamili za kadi au taarifa binafsi za mtu mwingine bila ruhusa.

4. Watoa huduma na links za nje

Jukwaa hutumia Google kwa kuingia, Supabase kwa uthibitisho na database, pamoja na huduma za hosting na assets za ukurasa. Watoa huduma hao huchakata taarifa zinazohitajika kuendesha sehemu zao kwa masharti yao; uchakataji unaweza kufanyika nje ya Tanzania. Links za materials zinaweza kukupeleka kwenye huduma za watu wengine, ambapo ruhusa na sera za mwenye faili hutumika.

Unaweza kusoma sera ya Google na sera ya Supabase. RUCUSO haiombi ufikiaji wa data nyingine ya Google kwa ajili ya matangazo.

5. Session na hifadhi ya kivinjari

Kivinjari kinaweza kuhifadhi session ya kuingia, taarifa za uthibitisho uliopita na mapendeleo ya muonekano. Sehemu ya chat hutumia alama ya muda ili kukurudisha baada ya Google login. Unaweza kutoka kwenye akaunti na kufuta hifadhi ya website kwenye kivinjari; kufanya hivyo hakufuti moja kwa moja rekodi zilizotumwa kwenye database.

6. Uhifadhi, marekebisho na kufuta taarifa

Kwa sasa mfumo haujaweka muda mmoja wa kufuta rekodi zote kiotomatiki. Rekodi hutumika kuendesha huduma, kufuatilia masuala na usimamizi wa mfumo. Unaweza kuwasiliana na RUCUSO kuomba kufikia, kusahihisha au kufuta taarifa zako au akaunti. Ombi litahitaji kuthibitisha utambulisho wako na kupitiwa na msimamizi, ikiwemo kuangalia rekodi zinazohusiana na kesi na ujumbe. Nakala za kiufundi zinaweza kufuata taratibu za watoa huduma.

Kuondoa ruhusa ya RUCUSO kwenye akaunti yako ya Google hakufuti moja kwa moja rekodi ulizotuma kwenye RUCUSO. Kwa ombi la taarifa, akaunti au faragha, tumia Mawasiliano ya RUCUSO au wasiliana na uongozi wa RUCUSO chuoni. Usitume password au msimbo wako wa siri kwenye mazungumzo ya group.

7. Mabadiliko ya sera

Toleo lililosasishwa litawekwa kwenye ukurasa huu pamoja na tarehe yake. Soma sera hii tena unapochagua kutumia huduma mpya au kuchapisha taarifa.

Sample za malipo ya mkopo Pending

Fomu hii hukusanya majina matatu, registration number, Form Four Index Number, jina la benki na namba ya akaunti kwa ridhaa yako. Taarifa ni za ufuatiliaji wa changamoto ya malipo na zinasomwa na Waziri na Naibu wa Mikopo na super admin pekee. Hatukusanyi PIN, CVV, OTP au namba ya kadi. Mfumo hauunganishwi na benki au HESLB kuthibitisha malipo. Akaunti inaoneshwa sehemu tu kwenye orodha; kufungua namba kamili na kupakua orodha hurekodiwa kwenye log ya ndani. Rekodi inayorudiwa haiwezi kubadilisha akaunti iliyowasilishwa awali; kwa marekebisho wasiliana na wahusika wa Wizara ya Mikopo. Wahusika wahifadhi na kushiriki faili za ufuatiliaji kwa madhumuni haya tu.